Kenyans Live

Idara ya mahakama yasema iko tayari kukabiliana na kesi ibuka za uchaguzi

Description (show more)

Jaji mkuu Martha Koome ametoa hakikisho kwa taifa kwamba kwamba idara ya mahakama iko tayari kushughulikia migogoro yoyote ya kisheria itakayoibuliwa na uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, kwa muda ulioratibiwa. Kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa, Jaji mkuu alitangaza kuwa mpango wa utoaji mafunzo kuhusu migogoro ya uchaguzi kwa awamu utaanza wiki hii. Mpango huo utakaoongozwa na taasisi ya mafunzo kwa maafisa wa idara ya mahakama na kamati ya uchaguzi ya idara hiyo, unawalenga maafisa zaidi ya 400 wakiwemo majaji, maafisa wa mahakama na wafanyakazi wa idara hiyo. Koome aliwahakikishia wakenya kwamba idara hiyo itazingatia usawa na haki wakati wa kushughulikia migogoro ya uchaguzi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: