Kenyans Live

Padre Nyangeri apaza sauti dhidi ya pombe haramu Nyamira

Description (show more)

Padre mmoja katika Kaunti ya Nyamira ameanzisha kampeni ya kipekee dhidi ya pombe haramu, akisema amechochewa na vifo vya mara kwa mara vinavyohusishwa na unywaji wa pombe hiyo. Padre huyo amekuwa akihamasisha jamii kuhusu madhara ya pombe haramu na sasa ameahidi kuendelea kupaza sauti hadi hatua kali zichukuliwe dhidi ya wanaouza pombe hiyo. Kama anavyoripoti Maryanne Nyambura, Padre Bernard Nyangeri wa Kanisa Katoliki la Rangenyo anasema vita dhidi ya pombe haramu vinahitaji hatua madhubuti ili kukabiliana na tatizo hilo.

Share: