Kenyans Live

Uamuzi wa kesi kuhusu IEBC kukosa kuratibisha mipaka kutolewa mwakani

Description (show more)

Mahakama kuu jijini Nairobi , mnamo tarehe 25 mwezi februari mwaka ujao itatoa uamuzi wa ombi lililowasilishwa na wakili Philip Kipkemoi Langat la kulalamikia kukosa kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka kuchunguza upya mipaka ya maeneo bunge na wadi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.Wakili huyo anadai tume ya IEBC ilikiuka kifungu nambari 89 cha katiba  kwa kukosa kuandaa shughuli ya lazima ya  kuchunguza upya mipaka hiyo katika muda unaohitajika wa kati ya miaka 8 na 12 baada ya kufanywa mara ya mwisho mwaka 2012. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: