Kenyans Live

Wakazi wa Lamu waandamana kupinga kiwanda cha Dangote

Description (show more)

Huku Rais William Ruto akitarajiwa kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kusafishia mafuta ghafi cha Dangote East Africa hapo kesho katika Kaunti ya Lamu, wakazi wa kaunti hiyo wameendeleza maandamano wakilalamikia kutohusishwa kikamilifu kabla ya mradi huo kuanza. Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kutawanya umati huo, ambao ulisisitiza kuwa sharti sheria ifuatwe na wapewe haki yao. Kama anavyoarifu Laura Otieno, wakazi hao wameishutumu serikali wakidai hawana imani kuwa watafidiwa wala kwamba mradi huo utawanufaisha.

Share: