Kenyans Live

Kenya yaweka mikakati ya kuongeza idadi ya swara aina ya Mountain Bongo

Description (show more)

Kenya inalenga kuongeza idadi ya swara aina ya Mountain Bongo kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, huku ikiimarisha juhudi za kuokoa mnyama huyo aliye hatarini anayepatikana nchini Kenya pekee. Mpango wa pili wa Kitaifa wa Urejeshaji na Hatua za Uhifadhi uliozinduliwa Nanyuki, unalenga kulinda misitu, kuboresha uzalishaji wa bongo walio kifungoni na kuwaachilia porini, pamoja na kushirikisha jamii katika uhifadhi.

Share: