Kenyans Live

Safaricom: Uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za serikali ulikamilishwa

Description (show more)

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imesema uuzaji wa asilimia 15 ya hisa zinazomilikiwa na serikali ulikamilishwa tarehe 30 Juni mwaka huu. Kauli hiyo inajiri huku Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi akisisitiza kuwa uuzaji wa hisa hizo ulifanywa kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia maslahi ya kifedha ya taifa. Serikali imeazimia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliobatilisha uuzaji wa hisa hizo kwa kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini.

Share: