Kenyans Live

Uhuru Kenyatta adai Hayati Raila Odinga alishinda uchaguzi wa uraia wa 2022

Description (show more)

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anasema anaamini kuwa Hayati Raila Odinga alishinda katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2022, licha ya Mahakama ya Upeo kuthibitisha ushindi wa Rais William Ruto. Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Jubilee, Kenyatta pia amewashtumu wanaodai kuwa hakufanya lolote kumsaidia Hayati Raila, akimkashifu Rais Ruto kwa kuzidi kumshambulia. Kenyatta anasema Ruto anamtumia kama kijisababisho kwa sababu ameshindwa kutekeleza aliyowaahidi Wakenya.

Share: