Kenyans Live

Seneti yamuenzi Fred Obachi Machoka kwa miaka 50 ya utangazaji

Description (show more)

Bunge la Seneti limemuenzi mtangazaji tajika wa Royal Media Services, Fred Obachi Machoka, anayeadhimisha miaka 50 katika tasnia ya utangazaji. Maseneta wamewahimiza Wakenya kuhudhuria tamasha la kuadhimisha miaka 50 ya utangazaji wa Machoka, litakalofanyika Jumamosi, tarehe 10, katika Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi. Machoka, aliyeandamana na watangazaji wengine wakongwe katika Seneti, alisifiwa kwa weledi na uchapakazi wake katika tasnia ya utangazaji.

Share: