Kenyans Live

Watetezi wa haki wataka hatua dhidi ya polisi waliomkamata mwanahabari Ode Francis

Description (show more)

Kundi la watetezi wa haki za kibinadamu linataka Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi, IPOA, na Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI, kuwachukulia hatua maafisa wa usalama waliomkamata kwa muda mwanahabari wa Citizen TV, Ode Francis. Kundi hilo linasema kuvamiwa na kukamatwa kwake alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya uanahabari ni unyanyasaji mkubwa. Limetaka uchunguzi wa kina kufanywa na maafisa husika kuwajibishwa. Kundi hilo limetoa makataa ya siku saba kwa hatua kuchukuliwa. Kama anavyoripoti Serfine Achieng Ouma.

Share: