Kenyans Live

Mbadi apuuzilia mbali madai ya njama ya kunyakua hisa za KPC

Description (show more)

Waziri wa Hazina ya Kitaifa, John Mbadi, amepuuzilia mbali madai ya kinara wa chama cha The People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, kwamba kuna njama ya kunyakua hisa za kampuni ya kusambaza mafuta nchini, KPC, kupitia mfanyabiashara Aliko Dangote. Akizungumza na runinga ya Citizen, Mbadi amesema ununuzi wa hisa za KPC uko wazi kwa wote. Kama anavyoripoti Emmanuel Too, Mbadi alimkashifu Nyoro, akisema anajitafutia tu umaarufu wa kisiasa.

Share: