Kenyans Live

IPOA kuwahoji maafisa saba wa polisi kuhusu madai ya kumshambulia mwanahabari wa Citizen TV

Description (show more)

Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) inatarajiwa kuwahoji zaidi ya maafisa saba wa polisi kuhusiana na madai ya kumshambulia na kumkamata kwa nguvu mwanahabari wa Citizen TV, Ode Francis. Miongoni mwa maafisa watakaohojiwa ni OCPD na OCS wa Kituo cha Polisi cha Central, pamoja na maafisa watano wanaodaiwa kumkamata Ode. Mwanahabari huyo tayari amerekodi taarifa yake kwa IPOA kuhusu tukio hilo lililotokea Jumanne.

Share: