Kenyans Live

Mwanamke ashtakiwa kwa madai ya kumuibia mwajiri

Description (show more)

Mwanamke mwenye umri wa miaka 32 ameshtakiwa kwa wizi wa zaidi ya shilingi milioni moja kutoka kwa kampuni iliyokuwa imemwajiri kama muuzaji bidhaa. Akiwa mbele ya hakimu mkuu. Abdul Lorot katika mahakama ya Makadara jijini Nairobi, Anne Muthoni Mugambi alikanusha shtaka la wizi kinyume cha sheria. Inadaiwa kwamba katika siku tofauti kati ya Januari mosi na Mei 15 mwaka huu jijini Nairobi akiwa muuzaji bidhaa katika kampuni ya East Com Tech Alnoor Digital, aliiba shilingi milioni 1,042,000. Alikanusha shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja pesa taslimu. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: