Kenyans Live

Polisi wakwamisha maandamano ya kudai kuachiliwa kwa Besigye Nairobi

Description (show more)

Hali ya taharuki ilishuhudiwa jijini Nairobi mapema leo baada ya polisi kuvuruga mipango ya maandamano ya wanaharakati waliokuwa wakitaka mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Daktari Kizza Besigye, aachiliwe. Waandamanaji wanne walikamatwa walipokuwa wakijaribu kuelekea Barabara ya Harambee, wakilenga kuandamana hadi Ofisi ya Rais na Wizara ya Masuala ya Kigeni. Wanaharakati hao wanadai serikali ya Kenya inapaswa kuwajibishwa kwa kuwa Besigye alikamatwa akiwa nchini Kenya. Wakati huo huo, wanaharakati wanasema afya ya Besigye inazidi kudhoofika akiwa kizuizini.

Share: