Kenyans Live

Serikali yaahidi kupunguza ushuru wa mishahara kwa wenye mapato ya chini kufikia Novemba

Description (show more)

Si mara ya kwanza kwa serikali kuahidi kupunguza ushuru wa mishahara kwa Wakenya wanaopata mapato ya chini. Miezi minne baada ya ahadi hiyo kutolewa, Rais William Ruto amelirejelea suala hilo wakati wa sherehe za Mashujaa Day zilizofanyika Jumanne. Waziri wa Hazina ya Kitaifa, John Mbadi, sasa amesema kuwa sheria itakayowezesha utekelezaji wa pendekezo hilo inatarajiwa kuidhinishwa kufikia mwisho wa mwezi Novemba. hatua hiyo inalenga kuwezesha kupunguzwa kwa mzigo wa ushuru kwa wafanyakazi wenye mapato ya chini.

Share: