Kenyans Live

Familia ya Raila yatangaza kamati ya maadhimisho ya kumbukumbu

Description (show more)

Familia ya hayati Raila Odinga imetangaza kuundwa kwa kamati ya kitaifa itakayoongoza maadhimisho ya kumbukumbu yake kuanzia tarehe 10 Oktoba hadi tarehe 17 Oktoba. Balozi Mama Ida Odinga, mjane wa Raila, amesema kamati hiyo itajumuisha serikali kuu, vyama vya kisiasa, wasomi na Wakenya wote walioenzi maisha ya marehemu. Kamati hiyo itasimamiwa na Profesa Adams Oloo, huku aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Amos Wako, na Afisa Mkuu wa Telkom, Mugo Kibati, wakiwa miongoni mwa wajumbe.

Share: